Loading...

Wanawake 16 watekwa nyara na Boko haram huko Nigeria


Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamewateka nyara wanawake 16 katika eneo la mashambani kaskazini mashariki mwa jimbo la Adamawa huko Sabon Garin Madagali.
>>NEW AUDIO-Vanessa Mdee-niroge Download hapa
Wakaazi wanasema kuwa wanawake hao walitekwa msituni walipokuwa wakitafuta kuni na kuvua samaki katika mto chini ya ulinzi wa vijana wawili wa kuweka usalama wanaolisaidia jeshi dhidi ya wapiganaji hao.

BAADA YA UKIMYA TANGU SUKARI KUTOKA NJE KUZUIWA, BEI MPYA YA SUKARI YATANGAZWA RASMI.....



HATIMAYE  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli  imekisikia kilio cha muda mrefu  cha Wananchi ambao  walikuwa wakilalamika kupanda  kwa  bei ya sukari nchini. 

..sifa 10 za mpenzi mwaminifu 

.TB Joshua aonyesha maajabu

Akizungumza na Waandishi wa Habari  mchana huu  jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  mkuu wa Bodi ya Sukari nchini Tanzania, Henry Semwaza amesema kuanzia sasa kilo moja ya  sukari itauzwa sh.  1800 nchi nzima. 

"Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja
. "Amesema Semwaza na kuongeza;

" Wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi.

Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale wote watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo.


DC KANDA MAALUM YA DAR, MAKONDA AAGIZA WALIMU SHULE ZA MSINGI DAR KUPANDA DALA DALA BURE...




Kimsingi ni ndoto hii ya Mheshimiwa Raisi ambayo nina hakika kila mmoja wetu anaelewa ukubwa wa faida zake kwenye ujenzi wa Tanzania mpya na yenye wasomi na wataalamu wa kila namna tena wanaopatikana bila kuzingatia hali ya kipato cha familia anayotokea mwanafunzi, iliyonifanya mimi kama msaidizi wake katika nafasi ya ukuu wa wilaya nijiulize kila wakati juu ya ushiriki wangu wa kuhakikisha                                                                        inatimia kikamilifu. 
Maswali ambayo yamenifikisha kwenye wazo la kuboresha sekta hii kwa kuchagua kufanya jambo ambalo wakati serikali ikiendelea kupigania changamoto nyinginezo za kuboresha ajira za walimu ikiwemo upandishwaji wa madaraja na mishahara, basi na mimi katika nafasi yangu nishiriki kwenye mchakato huu mzima kwa kutoa motisha ya usafiri wa bure kwa walimu wote wanaofundisha kwenye shule za serikali zilizopo jijini Dar es Salaam.

Kwa ufupi ni kwamba, wazo hili limejengwa juu ya msingi wa sababu kubwa tatu. Moja, kwa kuzingatia changamoto za nauli za mara kwa mara wanazolazimika kuzilipa walimu ili kuyafikia kwa wakati maeneo yao ya kufanyia kazi na pili, ni kuhakikisha mimi na serikali yangu ya wilaya ya Kinondoni tunakuwa sehemu ya juhudi za Mheshimiwa Raisi za kuboresha maslahi na mazingira ya walimu ya kufanyia kazi ili matarajio ya ndoto yake anayoipigania usiku na mchana ya kutaka kuiona sekta ya elimu nchini ikikua kwa kasi yanatimia. 
Na tatu, ni kuwafanya walimu wa wilaya ya Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla kama watumishi wenzangu wa serikali nao wanafaidi sehemu ya matunda ya serikali yao ambayo kwa dhati imedhamiria kubadilisha maisha yao ili na wao waweze kubadilisha maisha ya vijana wetu kupitia taaluma.

Kwasababu hizo nilizozianisha hapo juu ninaomba kuwatangazia walimu wangu wa shule zote za serikali kuanzia za msingi mpaka sekondari ya kwamba, sasa watasafiri bure wanapokwenda kutufundishia wadogo zetu na watoto wao. 
Hii ni baada ya kufanya vikao na mazungumzo ya kina na wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma kupitia vyama vyao vya Darcoboa na Uwadar na hatimaye mazungumzo hayo kuitimishwa na mkutano wa vyama vyote hivyo viwili vya wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao kwa sauti moja wamekubali kuniunga mkono kwenye utekelezaji wa wazo langu hili.

Kipekee na kwa unyenyekevu mkubwa, naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wamiliki hawa wa vyombo vya usafiri wa umma pamoja na viongozi wa vyama vya Darcoboa na Uwadar kwani walikuwa na kila sababu ya kukataa hasa ukizingatia kuwa wao ni wafanyabiashara na tena wanazo changamoto nyingi katika sekta yao ya usafirishaji, wengine wakiwa hata wamekopa kwenye mabenki ili wapate uwezo wa kufanya biashara, lakini kwenye jambo hili wote kwa umoja wao wameseme ndio na wako tayari kuanza haraka iwezekanavyo.
© Copyright UHONDO WA MTAA | Modified By PB Web and Graphics
Back To Top